Bernardino Realino

Masalia yake huko Lecce.

Bernardino Realino, S.J. (Carpi, Emilia-Romagna, 1 Desemba 1530Lecce, Puglia, 2 Julai 1616) alikuwa padri wa Italia na mtawa wa Shirika la Yesu maarufu kwa mahubiri yake, kwa toba na kwa huduma zake kwa maskini, wagonjwa na wafungwa [1][2][3]

Kabla ya hapo alisomea sheria na kufanya kazi serikalini[4].

Realino alitangazwa mwenyeheri na Papa Leo XIII mwaka 1896, halafu mtakatifu na Papa Pius XII tarehe 22 Juni 1947.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Julai[5].

  1. Saint Bernadine Realino. Saints SQPN (12 June 2016). Retrieved on 8 November 2016.
  2. St. Bernardino Realino. Catholic Exchange (2 July 2016). Retrieved on 8 November 2016.
  3. Saint Bernardino Realino. The Jesuit Curia in Rome. Retrieved on 8 November 2016.
  4. Saint Bernardino Realino. Santi e Beati. Retrieved on 8 November 2016.
  5. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy